12 Sep 2019 / 54 views
Amunike awashtaki TFF kwa FIFA

Aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Emmanuel Amunike amelishtaki shirikisho la soka la Tanzania (TFF) kwa shirikisho la soka duniani FiFa akilalamikia kutolipwa haki yake.

Kocha huyo raia wa Nigeria ameamua kuwasilisha malalamiko hayo kwa Fifa ili kutafuta haki yake kwa kulipwa madai yake.

Amunike alitimuliwa na shirikisho la soka la Tanzania baada ya Tanzania kupata matokeo duni katika kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu nchini Misri .

Katika fainali hizo taifa Stars ilishika mkia kwenye kundi C lililokuwa na Senegal, Kenya, na Algeria baada ya kupoteza mechi zote tatu.

Kushindwa kwa Kenya ndio kulikohuzunisha wengi kwa kuwa walipoteza uongozi waliokuwa nao wa 2-0 kufikia kipindi cha mapumziko.

Na kufuatia matokeo hayo Amunike alisea kwamba timu hiyo ilihitaji uzoefu wa mashindano makubwa na kwamba wachezaji walihitaji kushiriki katika ligi zenye ushindani mkubwa ili kuweza kuimarika.

Kocha huyo ambaye mwenye umri wa miaka 47 ambaye hakuwa na kazi tangu alipoondoka klabu ya Sudan ya Al Khartoum mnamo mwezi Machi alisaini mkataba wa miaka miwili kwa kuifundisha Tanzania akichukua nafasi ya Salum Mayanga.

Amunike alishinda kombe la Afrika akiichezea Nigeria mwaka 1994 na mshindi wa dhahabu ya Olimpiki miaka miwili baadaye 1996.