12 Sep 2019 / 12 views
Kompani aagwa Man City

Gary Neville, Ryan Giggs na Ashley Cole walikuwa miongoni mwa nyota waliocheza kwenye mechi ya kumuaga mchezaji wa zamani wa Manchester City, Vincent Kompany.

Mechi hiyo kwa ajili ya kumuaga Kompany ilihusisha wachezaji wakongwe waliocheza Manchester City pamoja na mchanganyiko wa wachezaji waliocheza ligi kuu soka nchini Uingereza na matokeo yalikuwa 2-2.

Kocha wa wachezaji wakongwe wa zamani wa Manchester City alikuwa Pep Gurdiola huku kocha wa wachezaji wa zamani waliocheza ligi kuu alikuwa kocha wa sasa wa Ubelgiji, Roberto Matnez.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye kwasasa amejiuna na Anderlecht katika msimu wa joto, hakucheza kwenye mechi hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Etihad kutokana na kuwa majeruhi.

Martin Petrov ndiyo alikuwa wa kwanza kuipatia City goli la kwanza lakini Robbie Keane akasawazisha goli hilo.

Robin van Persie aliifungia timu ya wakongwe waliocheza ligi kuu nchini Uingereza ambapo goli hilo likaja kusawazishwa na Benjani Mwaruwari baada ya kuunganisha kichwa.

Pesa iliyopatikana kwenye mechi hiyo itapelekwa Tackle4MCR na itasaidia watu wenye mahitaji maalumu pamoja na watu wasiokuwa na makazi.

City wameamuru sanamu ya Kompany ijengwa nje ya Etihad, wakati barabara ndani ya uwanja wa mazoezi ya Klabu hiyo imepewa jina Vincent Kompany Crescent.