12 Sep 2019 / 12 views
Valencia yamfukuza kocha wao

Klabu ya Valencia imemfungashia vilago kocha mkuu wa timu hiyo, Marcelino Garcia na imemteua Albert Celades kuwa kocha mpya wa timu hiyo.

Marcelino Garcia amefukuzwa kufuatia maelewano mabovu na mmiliki wa klabu na amefukuzwa kutoka kwenye ripoti iliyotoka kwa mmiliki wa klabu Peter Lim.

Marcelino aliteuliwa kama kocha wa Valencia mnamo Mei 2017, msimu uliopita alifanikiwa kubeba kombe la Copa del Rey dhidi ya Barcelona pia kumaliza nafasi ya nne msimu uliopita, kwa msimu huu Valencia wamechukua alama nne kwenye michezo mitatu waliocheza mpaka sasa.

Kocha mpya ataanza na Barcelona pale Nou Camp Jumamosi na Jumanne dhidi ya Chelsea katika mchezo wao wa ufunguzi wa Ligi ya mabigwa.