11 Sep 2019 / 16 views
Zimbabwe yatinga makundi

Timu ya taifa ya Zimbabwe imefuzu hatua ya makundi michuano ya kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar baada ya kuwafunga Somalia 3-1 kwenye mechi iliyofanyika jana nchini Zimbabwe.

Zimbabwe wamefuzu hatua hiyo kwa jumla  3-2 kwa michezo yote miwili ambapo mchezaji nyota wan chi hiyo anayechezea klabu ya Kaizer Chiefs kushinda goli la ushindi kwenye mechi hiyo.

Somalia, ambao lazima utumia kucheza mechi zao nyumbani katika nchi nyingine ya Djibouti kwa sababu ya hali ya usalama huko Mogadishu walishinda mechi ya kwanza kwa bao 1-0.

Somalia ambayo ni timu ya taifa iliyoshika nafasi ya chini barani Afrika ilitaka kuingia makundi kufuzu michuano ya kombe dunia lakini wakatolewa jumla ya magoli 3-2.

Goli kutoka kwa Omar Abdullah Mohamed liliwapatia Wasomali fursa ya jumla ya 2-1 baada ya kusawazisha lakini wakafungwa dakika za mwisho za mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa taifa wa Zimbabwe.

Marshall Munetsi aliweka Zimbabwe mbele kwa dakika 77 baada ya kupiga shuti na kumshinda mlinda mlango wa Somalia na kutinga nyavuni.

Hiyo ni mechi ya pili kwa kocha mpya wa Zimbabwe, Joey Antipas ambaye mwezi uliopita alirithi timu hiyo baada ya kuondolewa kwenye michuano ya mataifa ya Afrika iliyofanyika nchini Misri.