14 Aug 2019 / 42 views
Man City yapigwa faini na Fifa

Manchester City imeepuka kufungiwa kusajili baada ya kukiri kuvunja sheria za shirikisho la soka duniani (FIFA) za usajili wa wachezaji vijana.

Licha ya kukiri mabingwa hao watetezi wa ligi kuu soka nchini Uigereza wamepigwa faini ya £315,000 kutokana na kuvunja sheria hiyo hivyo hawatofungiwa kusajili kutokana na uvunjaji wa sheria hiyo kwa wachezaji vijana.

Shirikisho la soka duniani ‘Fifa’ limesema kuwa Manchester City imevunja kanuni ya 19 kinachoruhusu mchezaji kijana lazima asajiliwe akiwa na umri zaidi ya miaka 18.

Manchester City wamesema kuwa wamekubali adhabu hiyo na watalipa faini hiyo kama ilivyoamuriwa na shirikisho la soka duniani kwenye adhabu hivyo wao kama timu wamekubali kulipa faini hiyo walioambiwa.

Mwaka jana wachezaji wawili kutoka kituo cha kulelea wachezaji ‘Right to Dream Football Academy ambao ni Dominic Oduro kutoka Ghana na George Davies kutoka Sierra Leone walisajiliwa na Manchester City na kucheza mechi za vijana kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.

Kamati ya nidhamu ya FIFA imeitaka Manchester City kutovunja sheria kuhusiana na usajili wa wachezaji wa wa umri chini ya miaka 18 na kufuata sheria za usajili zilizowekwa na shirikisho la soka duniani (FIFA).

Chelsea wamefungiwa na FIFA mwezi wa pili mwaka huu kutosajili wachezaji kwa miaka miwili baada ya kuvunja sheria ya shirikisho hilo kwa kwasajili wachezaji 29 kinyume na sheria hiyo ya shirikisho la soka duniani FIFA.