14 Aug 2019 / 30 views
Neymar kurejea Barcelona

Barcelona inatarajia kuwatoa wachezaji wake wawili, Phillipe Coutinho na Ivan Raktic kwenda PSG kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Neymar.

Barcelona ipo katika mipango ya kumrejesha Neymar kutoka PSG baada ya miaka miwili tu kupita tangu kujiunga na matajiri hao wa Ufaransa.

Mkurugenzi wa Barcelona alisafiri kuelekea Ufaransa kwaajili ya kufanya mazungumzo ya kumsajili nyota huyo raia wa Brazil ambaye ameonesha nia ya kuondoka katika klabu hiyo ya PSG kutoka jiji la Paris nchini Ufaransa.

Baada ya kutumia zaidi ya pauni Milioni 108 kumsajili Mfaransa, Antoine Griezman ilielezwa kuwa Barcelona ilikuwa na mpango wa kumchukua kwa mkopo Neymar ili kuepuka adhabu ya FIFA na hivyo kumsajili kwa dau kubwa msimu ujao.

Baada ya mazungumzo baina ya viongozi wa timu hizo mbili imeripotiwa kukubaliana kwa kuwatoa wachezaji wawili ili kubadilishana na Neymar.

Barca watawtoa wachezaji wake Philippe Coutinho na Ivan Rakitic ikiwa ni maombi ya PSG kutaka wachezaji hao ili wamuachia Neymar kurudi klabu yake ya zamani hivyo kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo akarejea Barcelona.