14 Aug 2019 / 49 views
Man U wakataa kumuuza Pogba

Maafisa wa Paris St-Germain na Barcelona walikutana kwa mara ya kwanza kujadili kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa PSG Neymar lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa baada ya mazungumzo ya saa tatu.

Barca wanajiandaa kutoa ofa kwa PSG ya kitita cha pauni milioni 93 pamoja na mshambuliaji Philippe Coutinho, 27 na kiungo wa Croatia Ivan Rakitic, 31, kumnasa Neymar.

PSG imeiambia Barca kuwa ofa ya pauni milioni 93, mchezaji Coutinho, Rakitic na beki wa kulia wa Ureno Nelson Semedo, 25, itatosha kumchukua Neymar.

Manchester United haitakubali ofa yeyote kwa kiungo Paul Pogba,26, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani ulaya.

United inaweza kumlipa Alexis Sanchez sehemu ya mshahara wake ikiwa mshambuliaji huyo, atakubali kuhamia Roma kwa mkopo.

Sanchez aligongana na mshambuliaji mwenzie Mason Greenwood baada ya kinda huyo,17, kumfanyia madhambi baada ya Sanchez kurejea kwenye mazoezi ya kwanza tangu alipopona majeraha.

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa timu ya taifa ya Ubelgiji Toby Alderweireld, 30 yuko tayari kumalizia mkataba wake na Tottenham ili aweze kuondoka kama mchezaji huru msimu ujao. (Mirror)

Mchezaji wa nafasi ya ulinzi Dejan Lovren, 30, alikosa mazoezi na timu ya Liverpool kujiandaa na mechi ya Jumatano ya kombe la Uefa, Super Cup wakati timu hiyo ikiwa imeanza mazungumzo kuhusu uhamisho na Roma.

Newcastle United wako kwenye mazungumzo kuhusu mkataba mpya kwa ajili ya kiungo Sean Longstaff, 21, baada ya Manchester United kuonesha nia ya kumpata mchezaji huyo.

Maafisa kutoka klabu ya Brazil, Flamengo wameelekea Ulaya kwa mazungumzo ya lengo la kumsajili mshambuliaji wa Italia na klabu ya Marseille Mario Balotelli, 29, kwa mkataba wa miaka miwili.

Manchester City imeepuka adhabu kama ya Chelsea ya kufungiwa kufanya usajili baada ya ''kukubali kuwajibika'' kuhusu kuvunja sheria kuwasajili wachezaji wadogo.

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge, 29, atafanya maamuzi kuhusu mustakabali wake juma hili wakati ambapo klabu 13 zimeonesha nia ya kumnyakua, huku klabu ya Uturuki Fenerbahce ikitangaza dau la pauni 60,000 kwa wiki.