14 Aug 2019 / 38 views
Ronaldo ataja tofauti yake na Messi

Mshambuliaji wa Juventus na Ureno, Cristiano Ronaldo ametaja kitu kinachomtofautisha kati yake na mpinzani wake mkubwa kwenye soka Lionel Messi.

Ronaldo wa Juventus na Lionel Messi wa FC Barcelona ndio wamekuwa wakishindanishwa kwa kiwango kikubwa, licha ya Ronaldo kukiri kuwa wao ni bora kutokana na kutawala tuzo za Ballon d’Or kwa miaka 10 kila mmoja akichukua mara tano ila mataji ya Ulaya yanawatofautisha.

“Nimekuwa mfungaji bora wa UEFA Champions League mara sita mfululizo, hakuna wachezaji wengi walioshinda Champions League mara tano hivi ndivyo ninavyoona naweza kujitambulisha mwenyewe katika mashindano haya.

Pia Messi ni mchezaji mzuri sio tu kwa kushinda Ballon d’Or mara tano bali kwa kuwa bora kama mimi kila mwaka.

Ronaldo amesema kuwa “Utofauti kati yangu na Messi ni kwamba nimecheza vilabu mbalimbali na kushinda Champions League nikiwa na club tofauti tofauti.

Ronaldo ametwaa mataji mengi zaidi ya kimataifa (2) Euro 2016 na UEFA National League akiwa na timu yake ya taifa ya Ureno wakati Messi hajawahi kutwaa taji lolote akiwa na Argentina.

Ronaldo ameshinda Champions League mara tano, nne akiwa na Real Madrid na moja akiwa na Manchester United  mwaka 2008 wakati Messi ameshinda mara nne tu akiwa na Barcelona.