13 Aug 2019 / 33 views
Bayern Munich wamsajili Perisic

Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich wamemsajili Ivan Perisic kwa mkopo kutokea klabu yya Inter Milan ya nchini Italia baada ya kukosa saini ya Leroy Sane kutoka Manchester City.

Perisic pia aliwahi kuchezea klabu za  Borussia Dortmund na VfL Wolfsburg katika ligi ya Ujerumani kati ya mwaka 2011 na 2015, mchezaji huyo anatarajia kuanza kucheza kwenye mechi ya ligi ya Bundersliga siku ya Ijumaa.

Mchezaji huyo ameletwa kwa ajili ya kuimarisha sehemu ya winga akisaidiana na Serge Gnabry na Kingsley Coman kufutia kuondoka wa wachezaji wakongwe wa klabu hiyo ambao walikuwa wanacheza naFasi hizo, Arjen Robben na Franck Ribery.

Pia Coman anasumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara toka alivyojiunga na timu hiyo miaka miwili iliyopiita hivyo ujio wa mchezaji huyo umekuja kuongeza nguvu kwa timu hiyo kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka nchini Ujerumani.

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich, Hasan Salihamidzic amesema kuwa mchezaji huyo atawasaidia msimu huu kutokana na kuwa na uzoefu wa muda mrefu kwenye michuano mbali mbali ya ndani nan je ya Ujerumani.

Salihamidzic amesema kuwa mchezaji huyo ana uwezo mkubwa akiwa uwanjani na ana uwezo wa kucheza nafasi ya winga vizuri hivyo ana uhakika wa kukopi na wachezaji wenzake kwasababu anaijua vizuri ligi ya Ujerumani pamoja na kocha Niko Kovac.

Bayern Munich walifungwa na Borussia Dortmund kwenye mechi ya kombe la Super Cup mwezi uliopita hivyo wanategemea kuanza kucheza mechi ya ligi kuu dhidi ya Hertha Berlin siku ya Ijumaa.