13 Aug 2019 / 23 views
Lamapard aionya Chelsea

Kocha wa Chelsea, Frank Lampard amewaonya wachezaji wake kuwa kamwe hatohitaji kuombwa msamaha hapo kesho siku ya Jumatano kama watapoteza mbele ya Liverpool mchezo wa fainali ya Super Cup.

Lampard ameyasema hayo wakati akiwa na kumbukumbu ya kupokea kipigo kizito cha mabao 4 – 0 dhidi ya Manchester United kwenye mchezo wake wa kwanza wa Premier League.

Kutokana na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Europa League msimu uliyopita Chelsea itakabiliana na mshindi wa taji la Champions League, Liverpool hapo kesho huko Istanbul.

 “Kila mchezaji atapaswa kuwa na uelewa juu ya umuhimu wa  huu mchezo ndani ya klabu hii, tumewapa kila kitu kwasababu utakuwa mgumu.”

Lampard mwenye umri wa miaka 41, akiwa kocha mpya wa Chelsea kwa mara ya kwanza anakutana na adhabu ya kutoruhusiwa kufanya usajili kwa misimu miwili huku akishuhudia nyota wake Eden Hazard akitimkia Madrid.

Wakati wakijipanga kwaajili ya kombe la Super Cup, Lampard ni kama mwenye mkosi kwani anakumbukwa akilikosa taji hili mwaka 1998.