13 Aug 2019 / 19 views
Bale kubakia Real Madrid

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 30 ataendelea kubaki Real Madrid akisubiri dirisha la usajili la ligi ya China kufunguliwa mwezi Novemba.

Manchester United wameshtushwa na taarifa kuwa Pogba anaweza kuachana na klabu hiyo msimu huu licha ya kuonesha kiwango cha hali ya juu kwenye mechi dhidi ya Chelsea.

Mabingwa wa Italia Juventus imezungumza na kiungo Christian Eriksen, 27, wakimtaka kujiunga na timu hiyo mkataba wake na Tottenham utakapomalizika mwishoni mwa msimu.

Bayern Munich wako kwenye mazungumzo na Barcelona kuhusu usajili wa kiungo wa Brazil Philippe Coutinho, 27, kwa mkopo.

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge, 29, atafanya maamuzi kuhusu mustakabali wake juma hili wakati ambapo klabu 13 zimeonesha nia ya kumnyakua, huku klabu ya Uturuki Fenerbahce ikitangaza dau la pauni 60,000 kwa wiki. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 26, alikubali kuweka kando tofauti yake na uongozi wa Crystal Palace baada ya mchezaji mwenzake Mamadou Sakho kumtaka ajitume walipokuwa kwenye mkutano wa wachzaji.

Wawakilishi wa kisheria wa mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Paris St-Germain, Neymar ,27, walionekana wakiingia katika ofisi za klabu yake ya zamani Barcelona.

Real Madrid imeendelea kuwa na nia ya kumsajili Neymar na kutamatisha nia ya kumsajili kiungo wa Manchaster United Paul Pogba, 26, ikiwa watampata mchezaji huyo.

Inter Miami itamsajili mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32, mkataba wake na PSG utakapokwisha mwezi Juni mwaka 2020.