13 Aug 2019 / 24 views
Polisi waanza kumchunguza Ronaldo

Polisi wa Korea Kusini wameanza kufuatilia suala la Cristiano Ronaldo kugomea kucheza mechi ya kirafiki kati ya Juventus dhidi ya mastaa wanaocheza Ligi Kuu Korea Kusini.

Mechi hiyo ilichezwa Julai 26 mwaka huu ambalo Ronaldo aligoma kucheza licha ya mkataba kudai kwamba angecheza kwenye mechi hiyo.

Promota wa mchezo huo aliahidi kuwa atacheza jambo lililofanya mashabiki wengi kununua tiketi ambazo zilikuwa bei ghali kwa ajili ya kuja kumuona Ronaldo kwenye mechi hiyo ya kirafiki lakini Ronaldo hakucheza.

Mashabiki walivamia ofisi za promota huyo wakitaka watajiwe sababu kwa nini nyota huyo hajacheza jambo lililofanya Polisi waweke usawa na kuwataka mashabiki kufungua kesi.

Mahabiki hao wamefungua kesi Polisi ya ulaghai kutokana na kile walichoahidiwa kutokamilika kwenye mechi hiyo ya kirafiki.

Baada ya mechi hiyo kumalizika mashabiki waliokuja uwanjani hapo kwa ajili ya kumuona Ronaldo walianza kuonesha hali ya hasira kutokana na mchezaji huyo kutocheza mechi hiyo licha ya kusainiwa mkataba.