12 Jul 2019 / 17 views
Kocha wa Ghana atakiwa kupewa nafasi

Mchezaji wa zamani wa Ghana, Mohammed Polo amesema kuwa kocha Black Stars Kwesi Appiah anastahili nafasi nyingine licha ya timu hiyo kutolewa mapema kwenye michuano ya mataifa ya Afrika mwaka huu.

Mashabiki wengi wa Ghana wamesema kuwa inatakiwa kocha huyo kuondoka kwenye timu hiyo baada ya kufanya vibaya kwenye michuano hiyo ya mataifa ya Afrika kwa mikwaju ya penati na Tunisia.

Hata hivyo Mohammed Polo amesema kuwa kwa upande wake ana imani Appiah ana nafasi ya kuendelea kuwa kocha mkuu wa timu hiyo licha ya kutofanya vizuri kwenye michuano hiyo ya mataifa ya Afrika.

“Tulikuwa na makocha wengi ambao wamefeli kufanya vizuri kwenye timu hii kama Appiah hivyo inatakiwa tumpe nafasi kwenye timu yetu ya Ghana” Alisema Polo.

“Ni bahati mbali amefanya vibaya kwenye michuano lakini aina mana kumfukuza kocha huyo kwasababu tumewekeza vya kutosha kwenye timu yetu pamoja na kocha mwenyewe hivyo tumpe nafasi”. Aliongeza Polo

Kocha Kwesi Appiah anaifundisha Black Stars kwa mara ya pili baada ya kuchaguliwa mwaka 2017 na kuwawezesha Ghana kufuzu michuano hiyo ya mataifa ya Afrika mwaka huu nchini Misri.