12 Jul 2019 / 26 views
Algeria yaipiga Ivory Coast

Timu ya taifa ya Algeria imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika kwa kuwafunga Ivory Coast penati 4-3 baada ya kutoka 1-1.

Algeria ilipata goli la kuongoza kupitia mchezaji Sofiane Feghoul kipindi cha kwanza cha mechi hiyo huku mchezaji wa timu huyo Baghdad Bounedjah akikosa penati kwenye dakika za kawaida.

Ivory Coast wakasawazisha goli hilo kupitia mshambuliaji wa Aston Villa, Jonathan Kodjia baada ya kupiga shuti na kumshinda kipa wa Algeria, Rais.

Ivory Coast ilikosa kosa kupata goli la pili baada ya jaribio la mchezaji Max Gradel kupanguliwa na kipa wa Algeria, Rais M'Bolhi dakika za mwisho za mchezo huo wa robo fainali ya michuano hiyo.

Mshambuliaji wa Crystal Palace, Wilfried Zaha ameonyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mechi hiyo baada ya kukosa nafasi za wazi kwenye lango la Algeria lakini jitihada zake hazikuzaa matunda kwenye mechi hiyo.

Baada ya ushindi huo, timu ya taifa ya Algeria itakutana na Nigeria kwenye mechi ya nusu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika siku ya Jumapili huku fainali ikichezwa Juni 19 mwaka huu.