11 Jul 2019 / 23 views
Madagascar kumenyana na Tunisia leo

Timu ya taifa ya Madagascar inashuka dimbani leo kumenyana na Tunisia kwenye mechi ya robo fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika.

Timu zote zimetinga hatua hiyo baada ya kuwaondoa wapinzani wao kwenye changamoto za mikwaju ya penati ambapo Tunisia waliwaondoa Ghana huku Madagascar ikiwaondoa DR Congo kwenye hatua ya 16 bora.

Madagascar ambayo ndiyo mara ya kwanza kushiriki michuano hii ya mataifa ya Afrika imeonyesha kiwango cha hali ya juu mpaka kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi lao lililokuwa na timu kubwa kama Nigeria.

Tunisia imefuzu hatua ya 16 bora kama best loser lakini ikafanya vizuri kwenye mechi ya hatua hiyo na kutinga robo fainali na kukutana na Madagascar.

Mshindi wa mechi hii atakutana na Senegal kwenye mechi ya nusu fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika baada ya Senegal kufuzu nafasi hiyo kwa kuwaondoa timu ya taifa ya Benin kwa goli moja kwa bila.

Mechi nyingine itakayochezwa leo ni kati ya Algeria atakayekipiga dhidi ya Ivory Coast kwenye mechi ya robo fainali mechi ambayo itakuwa ngumu na ya aina yake.