11 Jul 2019 / 23 views
Khazri apona majeraha

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tunisia, Wahbi Khazri amesema kuwa hana uhakika kama ataanza kwenye mechi ya leo ya robo fainali dhidi ya Madagascar japokuwa amepona majeruhi.

Khazri alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya misuli baada ya kuumia kwenye mechi ya hatua ya makundi dhidi ya Mauritania na kushindwa kuanza kwenye mechi ya hatua ya 16 bora dhidi ya Ghana.

Mchezaji huyo amesema kuwa kwasasa yupo vizuri kuelekea mechi hiyo ila maamuzi ya kumuanzisha kwenye mechi dhidi ya Madagascar yapo kwa kocha wake hivyo yeye anasikiliza maamuziki ya kocha.

“Sina uhakika kama nitaanza kwenye mechi dhidi ya Madagascar kwasababu anayepanga kikosi ni kocha kwa hiyo nasikiliza maamuzi ya kocha kuanza kwenye mechi hiyo dhidi ya Madascar”. Alisema Kharzi.

“Kwasasa tumefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo na tunatakiwa kuongeza nguvu zaidi kwenye mechi dhidi ya Madagascar” Aliongeza kusema mchezaji huyo.

Khazri ameshinda magoli mawili kati ya magoli manne yaliyofungwa na Tunisia kwenye michuano hiyo ya mataifa ya Afrika yanayoendelea nchini Misri.

Mshindi wa mechi hii kati ya Tunisia na Madagascar atakutana na timu ya taifa ya Senegal kwenye hatua ya nusu fainali baada ya Senegal kuwaondoa Benin kwenye mechi ya robo fainali.