11 Jul 2019 / 154 views
Kocha wa Nigeria alalamikia VAR

Kocha wa Nigeria, Gernot Rohr amesema kuwa mfumo wa VAR unatumia muda mwingi sana kutoa majibu kwenye mechi za kombe la mataifa ya Afrika nchini Misri.

Kocha huyo amesema hayo baada ya maamuzi ya VAR yaliyotolewa kwenye mechi ya robo fainali kati ya Nigeria na Afrika Kusini ambapo Nigeria alishinda 2-1 na kutinga hatua ya nusu fainali kwenye michuano hiyo.

Goli la Afrika Kusini lilifungwa na kiungo mchezaji wa timu hiyo, Bongani Zungu lakini likathibitishwa na VAR baada ya mchezaji huyo kuonekana kuotea lakini VAR ikathibitisha uhalali wa goli hilo.

Maamuziki ya goli hilo limechukua muda wa dakika tano kwa VAR kutoa maamuzi kitendo ambacho kocha wa Nigeria amelalamika kwasababu inachukua muda mrefu tofauti na VAR za sehemu nyingine.

Pia kocha huyo amewasifia wachezaji wake kwa kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo na kutinga hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Misri.

Mfumo wa VAR umeanza kutumika jana kwenye mechi za hatua ya makundi ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika ili kubaini makosa mbali mbali yanayotokea kwenye mechi za hatua hiyo.

Baada ya kushinda mechi hiyo Nigeria itakutana na mshindi kati ya Ivory Coast na Algeria ambao wanacheza leo kwenye mechi yao ya hatua ya robo fainali.