11 Jul 2019 / 24 views
Nigeria yatinga nusu fainali Afcon

William Troost-Ekong alifunga goli la dakika za mwisho na kuisaidia Nigeria kutinga nusu fainali ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Afrika Kusini.

Samuel Chukwueze alifunga goli la kwanza la Nigeria baada ya kupata krosi nzuri kutoka kwka Alexi Iwobi kabla ya kufunga baada ya jaribio la pili.

Bongani Zungu alisawazisha kupitia kichwa kilichodaiwa kuwa cha kuotea kabla ya refa wa Video VAR kusema kwamba mpira huo ulikuwa umemgonga mchezaji wa Nigeria kabla ya kumfikia.

Goli hilo ni la kwanza kwa mchezaji huyo wa Afrika Kusini toka kuanza kwa michuano hiyo ya mataifa ya Afrika nchini Misri mwezi Juni mwaka huu.

Mchezaji wa Udeneese Troost-Ekong alifika katika lango la Afrika Kusini katika muda uliotarajiwa na kuweza kucheka na wavu na hivyobasi kuisadia timu yake kufusu nusu fainali.

Baada ya kufuzu hatua hiyo ya nusu fainali Nigeria itakutana na mshindi kati ya Ivory Coast na Algeria ambao wanacheza leo hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Misri kwasasa.