10 Jul 2019 / 179 views
VAR kuanza kutumika Afcon leo

Mfumo wa Video Assistant Referee (VAR) utaanza kutumika leo kwenye mechi za hatua ya robo fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika nchini Misri ili kutambua makosa yatakayojitokeza katika mechi za hatua hiyo.

Hapo awali mfumo huo ulitakiwa kuanza kutumika katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo lakini wameamua kuanza kutumia hatua hii ili kupunguza lawama zinazotolewa na baadhi ya wachezaji kwenye michuano hiyo.

Makosa kadhaa ya kuzidi pamoja na mipira ya kushika ni moja wapo ya lawama zinazotolewa na baadhi ya wachezaji kwenye mechi za michuano hiyo.

VAR aikutumika kwenye mechi za awali kwasababu makosa yangekuwa mengi hivyo wameamua kuanza kutumia kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Misri kwasasa na timu nane zimetinga hatua ya robo fainali.

Mechi ya mzunguko wa pili wa michuano ya klabu bingwa Afrika ilishindwa kumalizika baada ya wachezaji wa klabu ya Wydad Casablanca kugomea mchezo huo kutokana na refa kukataa goli lao la halali kwenye mechi hiyo.

Rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad amesema kuwa wameamua kuanza kutumia VAR kwenye mechi za robo fainali ili kuzuia matatizo kwenye mechi hizo pamoja na lawama za wachezaji kwenda kwa waamuzi.