12 Jun 2019 / 36 views
Wchezaji 9 waliotemwa Taifa Stars

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Emmanuel Amunike amewaacha wachezaji tisa kwenye kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Misri.

Kocha huyo ameita kikosi hicho kamili leo akiwa nchini Misri kwa ajili ya kuwakilisha kwenye michuano hiyo ya mataifa ya Afrika itakayoanza Juni 21 mwaka huu.

Wachezaji waliotemwa ni pamoja na Shaban Chilunda, Miraji Athumani, Abdi Banda, Shiza Kichuya, David Mwantika, Selemani, Tangalu pamoja na makinda Kelvin John na Bonifase- Golikipa wa U18.

Kikosi hicho kitaongozwa na nahodha Mbwana Samatta ambaye anayechezea klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji ambayo ndiyo mabingwa wa nchini humo.

Tanzania kwenye michuano hiyo imepangwa katika kundi C pamoja na timu za Kenya, Senegal na Algeria, na mechi ya kwanza itacheza dhidi ya Senegal Juni 23 mwaka huu.