12 Jun 2019 / 36 views
Matarajiao ya Kenya Afcon

Timu ya taifa ya Kenya itacheza mechi ya kwanza katika michuano ya Afcon dhidi ya Algeria Juni 23 kabla ya kucheza na Tanzania Juni 27 mwaka huu.

Kiungo wa Harambee Stars, Eric Johanna amefunguka na kusema kuwa anaamini Kenya itafanya vizuri kwenye michuano hiyo kutokana na maandalizi makubwa waliyofanya kuelekea michuano hiyo.

Johanna ambaye anachezea klabu ya IF Brommapojkarna nchini Sweden amesema kuwa anajisikia vizuri kutokakana na maandalizi waliyofanya kwa ajili ya kuelekea michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.

Mchezaji huyo amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wanataka kuonesha tofauti kwenye michuano hiyo na watu kuzungumzia timu ya taifa ya Kenya baada ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Johanna amewataka mashabiki wa Kenya kuisapoti timu yao kwenye michuano ya kombe la mataifa ili wachezaji waweze kufanya vizuri kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Kenya imepangwa kundi C pamoja na timu za Algeria, Tanzania na Senegal kwenye michuano hiyo itakayoanza kuchezwa kuanzia Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu nchini Misri.