12 Jun 2019 / 26 views
Tunisia yaifunga Croatia 2-1

Tunisia imeifunga Croatia 2-1 katika mechi ya kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika kuanzia Juni 21 mwaka huu nchini Misri.

Tunisia ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli kuptia Anice Badri amabye anayechezea klabu ya Esperance dakika ya 16 ya mchezo huo, mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Tunisia alikuwa mbele kwa goli moja.

Bruno Petkovic aliisawazishia Croatia dakika 47 ya mchezo huo, Naim Sliti aliipatia Tunisia goli la pili dakika ya 70 ya mchezo huo na kuipa Tunisia ushindi kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika.

Tunisia ambaye ni bingwa wa Afrika mwaka 2004 ambapo alikuwa mwenyeji wa mwaka huo, kwasasa yupo kundi E pamoja na timu za Angola, Mali na Mauritania.

Pia Burundi ni timu nyingine ambayo inashiriki michuano ya kombe la mataifa mwaka huu kwa mara ya kwanza walicheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Algeria ambapo walitoka 1-1 kwenye mechi iliyofanyika Doha.

Magoli yote yaliingia kipindi cha pili ambapo Algeria walikuwa wa kwanza kupata goli dakika 39 ya mchezo huo na Burundi wakasawazisha baada ya golikipa Rais M’Bolhi kujifunga.