12 Jun 2019 / 33 views
Kikosi cha Namibia Afcon

Kocha wa timu ya taifa ya Namibia, Ricardo Mannetti ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya michuano ya mataifa ya Afrika Afcon.

Kwenye michuano hiyo, Namibia imepangwa kundi D pamoja na timu za Ivory Coast, Morocco na Afrika Kusini ambapo yeye ndiyo anaonekana dhaifu kwenye kundi hilo kutokana na ushiriki wake kwene michuano hiyo.

Kikosi kamili

Magolikipa: Ratanda Mbazuvara (African Stars), Loydt Kazapua (Maccabi FC, South Africa), Max Mbaeva (Golden Arrows, South Africa).

Mabeki: Ryan Nyambe (Blackburn Rovers, England), Larry Horaeb (Baroka FC, South Africa), Denzil Haoseb (Highlands Park, South Africa), Ivan Kamberipa (African Stars), Charles Hambira (Tura Magic), Riaan Hanamub (Jomo Cosmos, South Africa)

Viungo: Ananias Gebhardt (Tura Magic), Absalom Iimbondi (Tigers FC), Willy Stephanus, Petrus Shitembi (both Lusaka Dynamos, Zambia), Ronald Ketjijere, Marcel Papama (African Stars), Dynamo Fredericks (Black Africa), Deon Hotto (Bidvest Wits, South Africa), Joslyn Kamatuka (Cape Umoya United).

Washambuliaji: Benson Shilongo (Ismaily, Egypt), Peter Shalulile (Highlands Park, South Africa), Itamunua Keimuine (Dire Dawa City, Ethiopia), Manfred Starke (Carl Zeiss Jena, Germany), Isaskar Gurirab (Life Fighters).

Namibia itacheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Morocco Juni 23 na Juni 28 itacheza dhidi ya Afrika Kusini katika uwanja wa Al Salam na mechi ya mwisho watacheza dhidi ya Ivory Coast Julai Mosi mwaka huu.