12 Jun 2019 / 34 views
Benati awa nahodha wa Morocco Afcon

Beki wa klabu ya Al Duhail ya nchini Qatar, Medhi Benatia amechagulia kuwa mahodha wa timu ya taifa ya Morocco kwenye michuano ya mataifa ya Afrika Afcon nchini Misri.

Kocha wa Morocco, Herve Renard amesema kuwa ameamua kumpa unahodha mchezaji huyo kutokana na uwezo wake wa kupambana uwanja pamoja na uwamasishaji wake kwa wachezaji wenzake.

Kwenye michuano hiyo, Morocco imepangwa kundi D pamoja na timu za Ivory Coast, Namibia na Afrika Kusini ambapo timu mbili zitapita hatua inayofuata

Kikosi kamili cha Morocco

Magolikipa: Yassine Bounou (Girona), Mounir El Kajoui (Malaga), Ahmad Reda Tagnaouti (Wydad Casablanca)

Mabeki: Yunis Abdelhamid (Stade Reims), Medhi Benatia (Al Duhail), Manuel da Costa (Al Ittihad), Nabil Dirar (Fenerbahce), Achraf Hakimi (Borussia Dortmund), Noussair Mazraoui (Ajax Amsterdam), Romain Saiss (Wolverhampton Wanderers)

Viungo: Youssef Ait Bennasser (St Etienne), Younes Belhanda (Galatasaray), Mehdi Bourabia (Sassuolo), Mbark Boussoufa (Al Shabab), Karim El Ahmadi (Al Ittihad), Faycal Fajr (Caen), Hakim Ziyech (Ajax Amsterdam).

Washambuliaji: Nordin Amrabat (Al Nasr), Sofiane Boufal (Celta Vigo), Khalid Boutaib (Zamalek, Egypt), Youssef En-Nesyri (Leganes), Abderrazak Hamdallah (Al Nasr), Oussama Idrissi (AZ Alkmaar).