12 Jun 2019 / 27 views
Kikosi kamili cha Tanzania Afcon

Kocha wa Taifa Stars, Emmanul Amunike ametaja kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya michuano ya AFCON 2019 nchini Misri na kuwaacha wachezaji 9.

Kesho Taifa Stars itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo, timu ya taifa ya Misri na Juni 16 itacheza dhidi ya Zimbabwe.

Kikosi hicho ni hiki.

Makipa
Metacha Mnata (Mbao) Aishi Manula (Simba SC) Aron Kalambo (Tz Prisons)

Mabeki
Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Kessy (Nkana, Zambia), Vicent Philipo (Mbao), Gadiel Michael (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Ally Mtoni(Lipuli), Erasto Nyoni (Simba), Agrey Moris (Azam).

Viungo
Feisal Salum (Yanga), Mudathir Yahya (Azam), Frank Domayo (Azam), Himid Mao (Petrojet, Misri), Yahya Zayd (Ismaily, Misri), Farid Mussa (Tenerife, Hispania)

Washambuliaji
Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Simon Msuva (Difaa El Jadid, Morocco),Abdilahie Abdallah Mussa (Blackpool, England), Thomas Ulimwengu (JS Soura, Algeria), John Bocco (Simba),Rashid Mandawa (BDF XI,Botswana).

Kwenye michuano hiyo, Tanzania imepangwa kundi C pamoja na timu za Kenya, Algeria na Senegal, na mechi ya kwanza itacheza dhidi ya Senegal Juni 23 mwaka huu.