12 Jun 2019 / 49 views
Salah kuiongoza Misri Afcon

Kocha wa timu ya taifa ya Misri, Javier Aguirre ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika Afcon yatakayoanza Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu.

Kikosi cha Misri kitaongozwa na mchezaji wa klabu ya Liverpool, Mohamed Salah ambaye ametoka kushinda ubingwa wa Ulaya karibuni dhidi ya Tottenham.

Kikosi Kamili

Magolikipa: Mohamed El Shenawy (Al Ahly-Misri), Ahmed al-Shennawy (Pyramids-Misri) na Mahmoud Abdelrahim Genesh (Zamalek-Misri)

Mabeki: Ahmed Elmohamady (Aston Villa/ENG), Omar Gaber (Pyramids), Ayman Ashraf (Al Ahly), Mahmoud Hamdy el-Winsh (Zamalek), Baher ElMohamady (Ismaily), Ahmed Hegazi (West Bromwich Albion/ENG), Ahmed Ayman Mansour(Pyramids), Mahmoud Alaa (Zamalek)

Viungo: Waleed Soliman (Al Ahly), Abdullah al-Saeed (Pyramids), Mohamed Elneny (Arsenal/ENG), Tarek Hamed (Zamalek), Ali Ahmed Ghazal (Feirense/POR), Mahmoud Hassan Trezeguet (Kasimpasa/TUR), Amr Warda (Atromitos/GRE), Nabil Emad Donga (Pyramids), Mohamed Salah (Liverpool/ENG)

Washambuliaji: Marwan Mohsen (Al Ahly-Misri), Ahmed Hassan Kouka (Olympiacos/Ugiriki), Ahmed Ali Kamel (Al Mokawloon-Misri). Mechi ya kwanza Misri itacheza dhidi ya Zimbabwe Juni 21 mwaka huu.